Breaking News

Muziki wa Nigeria unaendelea kupenya kila kona Duniani, Mchezaji wa zamani wa Manchester United Evra, akiimba wimbo wa Davido If (+ Video)

Ikiwa Tanzania inajitahidi kuupenyeza muziki wa Bongo Fleva katika kila kona ya dunia kwa wenzetu wa Nigeria mambo ni tofauti kwani tayari muziki wao unaitikisa dunia. Mbali na wasanii kama 2baba, P Square na wengine wakongwe waliofanikiwa kuupeneyeza muziki wao katika mataifa makubwa duniani kwa sasa wanaofanya vizuri katika mataifa makubwa barani Ulaya na hasa Katika taifa la Uingereza na Ufarasa bila kuisahau nchi ya Marekan ni Davido na Wizkid.


Nyimbo zao zimekuwa tishio sana na mara kwa mara tumemuona Davido akipost baadhi ya chat za muziki nchini Marekani zikionyesha nyimbo zake zinavyofanya vizuri lakini pia wimbo wake wa Fall ndio unaoongoza kwa kutazamwa na watu wengi zaidi katika mtandao Youtube lakini pia katika ukumbi mkubwa wa O2 Arena uliopo jijini London nchini Uingereza ni wasanii wawili tu kutoka Afrika waliowahi kuujaza ukumbi huo na hao sio wengine bali ni Davido na Wizkid wote kutoka Nigeria.





Kwenye mtadao wa Instagram wasanii hawa waonekana kupendwa sana barani Ulaya kwani siku za nyuma baadhi ya wachezaji wa Manchester United Pogba na Jesse Lingard walionekana kuucheza wimbo wa Come Closer wa Wizkid aliomshirikisha Drake na leo Clip iotembea ni ya mchezaji wa zamani wa Manchester United Patrice Evra akicheza wimbo wa avdo wa If.
Kwa habari za haraka na zauhakika zaidi endelea kutembelea website ya https://dirampya.blogspot.com/ ili uwe wa kwanza kupata habari.

No comments