Breaking News

Gari za abiria zapigwa marufuku kusafirisha vifurushi na barua

Niabu waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Mh Mhandisi Atashista Nditiye amepiga marufuku magari yote ya abiria kusafirisha vifurushi vya aina yoyote zikiwemo barua bila kuwa na leseni ya mamlaka ya mawasiliano nchini, huku akiitaka mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini nan chi kavu SUMATRA kuendesha oparationi kali kudhibiti vitendo hivyo.


Naibu Waziri Nditiye ametoa agizo hilo mjini Musoma mkoani Mara wakati akizungumza na watumishi taasisi mbalimbali ambazo ziko chini ya wizara hiyo ikiwemo kampuni ya simu nchini TTCL na shirika la Posta Tanzania.
Hata hivyo amewataka watendaji wa taasisi hizo kuziendesha taasisi hizo kwa faida, ikiwa ni pamoja na kutumia vema fedha zinatolewa na serikali kuu kama ruzuku,na kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa watendaji watakaobainika kwenda kinyume na maelekezo hayo.
Kwa habari za haraka na zauhakika zaidi endelea kutembelea website ya https://dirampya.blogspot.com/ ili uwe wa kwanza kupata habari.

No comments