Hatma ya Liverpool ni ipi katika mbio za ubingwa dhidi ya Manchester City PL ? kauli ya kocha “Hatuchezi PlayStation, bado tuna michezo 9”
Ikiwa ligi kuu nchini Uingereza PL inaendea mwishoni ikisalia takribani michezo 9 tu kumzika kwa ligi hiyo, kumekuwa na mchuano mkali kati ya timu mbili zinazopewa nafasi ya kutwaa taji la PL yaani Liverpool na Manchester City na mpaka sasa zikiwa zimepishana alama 1 tu Man city ikiwa na ma 71 na Liverpool wakiwa na alama 70.
![](https://bongo5.com/wp-content/uploads/2019/03/r-600x400.jpg)
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp kwa mara nyingi huwa ni mwingi wa bashasha na tabasamu – lakini sasa Je anakabiliwa na shinikizo kwa kutetereka kwa timu yake katika mpambano wa kulinyanyua taji katika ligi kuu England?
![](https://bongo5.com/wp-content/uploads/2019/03/HHH-600x341.jpg)
Timu hiyo imekuwa juu na kwa pointi saba mbele dhidi ya mabingwa Manchester City, ambao walikuwa wa pili walipokuwa wakielekea kwenye mechi Januari 3.
City ilishinda 2-1 na miezi miwili baadaye leo, Liverpool imeshuka kwa pointi moja nyuma ya wapinzani wao kufuatia mechi 8 za ligi nne kati yazo zikiishia kwa sare.
Timu ya Klopp ilikabiliwa na uhaba wa magoli dhidi ya wapinzani wao katika mechi ya derby iliyopita, na kulikuwa na ishara baada ya mechi kwamba shinikizo linamzidi Meneja huyo raia wa Ujerumani.
![](https://bongo5.com/wp-content/uploads/2019/03/105892659_klopp_ballboy_reuters-600x338.jpg)
Kufuatia mechi ya Jumapili huko Goodison Park, Klopp hakuwa na furaha alipomfuata muokota mpira ambaye kwa kejeli alimpigia makofi alipokuwa akitoka uwanjani.
Kwa mujibu wa BBC. Klopp aliondoka akitabasamu baada ya kujibizana kwa kifupi, lakini alikasirishwa na mwandishi habari ambaye baadaye aliyemuuliza swali kuhusu mtazamo wa timu yake dhidi ya Everton wakati wa mkutano na waandishi habari baada ya mechi.
![](https://bongo5.com/wp-content/uploads/2019/03/20160229001233822383-original-600x378.jpg)
“Hatuchezi Playstation,” amesema Klopp. “Unadhani hatukujiweka katika hatari ya kutosha leo? Je ndicho unachojaribu kuniuliza?
“Hilo ni swali la kuvunja moyo, kwa kweli.
“Bado kuna mechi 9. Hatuishiwi na subira kama nyinyi, hilo ni wazi. Ni mara ya pili unauliza swali ambalo kwa kweli silielewi”.
Mohamed Salah, aliyefunga mabao 17 ya ligi msimu huu, alipoteza nafasi mara mbili dhidi ya Everton na amefunga bao moja tu katika mechi zake saba zilizopita.
![](https://bongo5.com/wp-content/uploads/2019/03/bi-everton-cam-chan-klopp-noi-khung-trong-phong-hop-bao.jpg)
Hatahivyo, Klopp amesema athari ya kimbunga Freya, kilichochangia upepo mkali Uingereza Jumapili, ni sehemu ya sababu kwanini upande wake haukucheza vizuri katika mechi hiyo ya derby.
“Upepo hausaidii na ulikuwa mwingi leo. Ni lazima uwe tayari kwa mpambano wa pili ,” amesema meneja huyo wa Liverpool.
Ni mara ya pili katika miezi miwili iliyopita Klopp analaumu athari ya hali ya hewa kama sababu ya timu yake kung’ang’ana kutafuta magoli.
Hisia ya Jurgen Klopp imejitokeza ya ukaidi na pia ya matumaini baada ya mpambano dhidi ya Everton, akisisitiza kwamba bado kuna mechi 9 zilizosalia na changamoto bado ni nyingi katika njia hii ya kutafuta taji.
Hatahivyo Liverpool, inamuhitaji Mohamed Salah kutafuta upya angalau umahiri aliouonyesha msimu uliopita.
Manchester City ilionyesha kitisho cha kushuka kwa kasi yake baada ya kushindwa na Newcastle United mnamo Januari 29 lakini tangu hapo imejizatiti na kupata ushindi mara tano wa mechi za ligi na kudhihirisha upya nguvu yake.
![](https://bongo5.com/wp-content/uploads/2019/03/Screen-Shot-2018-12-26-at-16.57.14-600x375.jpg)
Bado Liverpool wapo kwa sana kwenye ushindani huu wa kulinyanyua taji, lakini hapakuwa na kubahatisha Goodison Park na ghadhabu ya wenzao kutoka upande wa pili wa Stanley Park wakati kipenga cha mwisho kilipopigwa.
No comments